Entertainment

Mr Seed akanusha kuwa tapeli mtandaoni

Mr Seed akanusha kuwa tapeli mtandaoni

Msanii kutoka nchini Kenya Mr Seed amekanusha tuhuma za kuwalaghai watu mtandaoni.

Akizungumza na Mungai Eve amesema madai hayo hayana ukweli wowote akisema kuwa yeye ni mfanyibiashara na mwekezaji wa sarafu ya bitcon.

Msanii huyo amesema hana ufahamu wowote kuhusu mtandao wa Send Wave Platform ambao anadaiwa kutumia kuwatapeli watu pesa zao.

Kauli yake imekuja mara baada ya baadhi ya wanawake kujitokeza na kudai Mr. Seed aliwaibia fedha zilizotengewa miradi ya uwekezaji wa nyumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *