
Mzazi mwenza wa msanii Mr Seed, Liz Sonia amemtuhumu msanii huyo kwa kukimbia majukumu ya kumlea mwanaye.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Liz amesema Mr. Seed amekuwa akikwepa majukumu yake kama baba kwa kipindi cha miaka saba iliyopita.
Aidha amesema kitendo cha Hitmaker huyo wa “Dawa ya Barida” kushindwa kutoa mahitaji ya msingi kwa motto wao ilimlazimu kujitolea kumhangaikia mwanaye ili aweze kukimu maisha yake.
Mrembo huyo amekiri kuchoshwa kubeba majukumu ya Mr. Seed ambaye amekuwa jeuri kwa muda mrefu huku akimuonya abadili miendo yake vingnevyo atakuja kujutia siku za mbeleni.