
Mwanamuziki wa injili aliyegeukia ukasisi kutoka nchini Kenya Mr. T amekiri kumuomba msamaha msanii wa nyimbo za injili nchini Tanzania Rose Muhando baada ya kumvunjia heshima mwaka wa 2021.
Kwenye mahojiano na mpasho Mr. T amesema alichukua maamuzi hayo baada ya watu kumshambulia kwenye mitandao ya kijamii ambapo amedai kwamba hakuwa na nia ya kumharibia jina Rose Muhando ila alikuwa anatoa mfano kwa wakristo.
Hitmaker huyo wa ngoma ya Finje Finje amesema hana ugomvi wowote na Rose Muhando akizingatiwa kuwa amekuwa akimtakia mema kwenye harakati za kuupeleka muziki wake kwenye hatua nyingine.
Mr. T aligonga vichwa vya habari nchini Kenya mara baada ya kumtolea uvivu Rose Muhando kwenye moja ya ibada yake ya kanisani kwa kusema kwamba anguko la Rose Muhando kimuziki lilikuja kufuatia hatua yake kujiunga na lebo ya muziki Sony Music.
Hata hivyo mashabiki wengi wa muziki wa injili Afrika Mashariki hawakufurahishwa na matamashi ya Mr. T jambo ambalo lilimlazimu Rose Muhando kujitokeza na kumsuta vikali kasisi huyo kwa kumharibia chapa yake ya muziki ambayo ameitengeneza kwa miaka nyingi.