
Baada ya wasanii kibao kutengeneza kiki kwa ajili kukamata attention ya mashabiki wao juu ya ujio wa kazi zao, Mwimbaji aliyegeukia ukasisi Mr. T yeye anapingana na kitendo hicho kwa kusema kwamba soko la muziki linakufa kwa njia hiyo.
Mr. T amefunguka na kusema kitendo cha wasanii kutengeneza kiki ili waweze kuzungumziwa katika media kuliko kazi zao inaua na kuwaharibu mashabiki kutokana na kufuatilia sana skendo za mastaa kuliko kazi zao.
Akizungumza na podcast ya Presenter Ali amesema kuwa kitendo hicho kimewaharibu wasanii wachanga ambao wanataka kutoka na kufikiria kuachia kiki kwanza ili wajulikane kwa haraka na kazi zao kuweza kufika mbali.
Hata hivyo amesisitiza kuwa ingawa kiki ina mchango kwenye muziki ila zifanyike kwa ustaarabu kwani inaweza kuwa shubiri pale wasanii wanapotupiana maneno machafu mtandaoni.