Entertainment

Msanii Chino Aomba Maombi Baada ya Kuugua Sana

Msanii Chino Aomba Maombi Baada ya Kuugua Sana

Msanii maarufu wa muziki anayefahamika kwa jina la Chino amewatia mashaka mashabiki wake baada ya kutoa taarifa ya kusikitisha kwamba anaumwa sana na kwa sasa anahitaji maombi kutoka kwa watu wote.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Chino hakufafanua kwa undani kuhusu hali yake ya kiafya, lakini alieleza kuwa anapitia kipindi kigumu na moyo wake unahitaji faraja na sala kutoka kwa wale wanaomjali.

Taarifa hiyo imezua hisia tofauti miongoni mwa mashabiki na watu wa karibu, huku wengi wakimiminika kumtakia ahueni ya haraka na kumtia moyo kupitia maoni na ujumbe wa matumaini.

Mashabiki na wapenzi wa muziki wake wameombwa kuungana kwa sala na dua ili Chino apate nafuu haraka na kurejea tena katika hali yake ya kawaida.

Tunaendelea kumtakia Chino uponyaji wa haraka na nguvu katika kipindi hiki kigumu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *