Msanii chipukizi wa Bongofleva Pipi Jojo ameachia rasmi EP yake mpya inayojulikana kwa jina “I Want To Make My Mama Proud”, kazi ambayo inajumuisha ngoma tano alizozifanya bila kumshirikisha msanii yeyote.
EP hiyo inajumuisha nyimbo kama “Chakacha,” “With You,” “Nakupenda,” “Waite,” na “Sunrise.” Kila wimbo una ladha yake ya kipekee, ikionesha ukuaji wa kimuziki na ubunifu wa msanii huyo anayejitengenezea jina kwenye muziki wa kizazi kipya.
Kwa mujibu wa Pipi Jojo, mradi huu ni wa kipekee kwani umetokana na ndoto yake ya kumfanya mama yake ajivunie mafanikio yake ya muziki kutokana na maisha magumu aliyokulia.
EP “I Want My Mama Proud” inapatikana kwenye majukwaa yote ya muziki mtandaoni, ikiwemo Spotify, Boomplay, na Apple Music.
Pipi Jojo ni msanii aliyeibuliwa na Chief God Love, ambaye amemkabidhi prodyuza Mr. T Touch jukumu la kumsimamia kisanaa ili kuhakikisha kipaji chake kinanawiri na kufika mbali zaidi.