Entertainment

Msanii Femi One Awapa Vijana Somo Kuhusu Maambukizi ya UKIMWI

Msanii Femi One Awapa Vijana Somo Kuhusu Maambukizi ya UKIMWI

Mwanamuziki kutoka Kenya, Femi One, ametoa wito kwa vijana nchini humo kuacha tabia ya kupima na macho wanapojihusisha na mahusiano ya kimapenzi.

Msanii huyo amesema kuwa ni muhimu kwa vijana kuwa waaminifu kwa wapenzi wao au kutumia kinga ili kujilinda dhidi ya maambukizi ya virusi vya HIV na magonjwa mengine ya zinaa.

Kupitia mtandao yake ya kijamii, Femi One amesisitiza kuwa mapenzi salama si suala la hiari bali ni jukumu la kila kijana.

Kauli yake imekuja baada ya takwimu za hivi karibuni kuonyesha kuwa idadi kubwa ya watu wanaoathirika na virusi vya UKIMWI nchini Kenya ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 34. Hali hii imeibua wasiwasi miongoni mwa wadau wa afya, ikizingatiwa kuwa kundi hilo ndilo tegemeo kubwa la taifa katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.  

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *