Others

Msanii Irene Ntale Akanusha Madai ya Vinka kuwa Meneja Wake

Msanii Irene Ntale Akanusha Madai ya Vinka kuwa Meneja Wake

Msanii kutoka nchini Uganda, Irene Ntale, amekanusha madai yanayoendelea kusambaa mtandao kuwa Vinka aliwahi kuwa meneja wake wakati akiwa chini ya lebo ya Swangz Avenue.

Akizungumza kwenye mahojiano maalum, Ntale amesema Vinka hakuwa meneja, bali alikuwa msaidizi wake binafsi katika majukumu ya kila siku ya kazi.

Ntale amesema wasimamizi wake halisi walikuwa wamiliki wa lebo hiyo, Kyazze na Benon, akisisitiza kuwa taarifa zilizoenea mitandaoni zilivuruga uhalisia wa majukumu yao.

Amesema pia alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kubaini kipaji cha Vinka kwani mara nyingi alimualika studio kwa mazoezi ya sauti, hatua iliyosaidia kuanzisha safari yake kwenye muziki. Ameongeza kuwa kabla ya kuanza kuimba, walikutana akiwa kama dansa na baadaye akagundua ana sauti nzuri yenye uwezo wa kukua.

Tetesi za awali zilidai kuwa Ntale aliondoka kwenye lebo ya Swangz Avenue kwa sababu Vinka alipendelewa na mabosi wa lebo hiyo, hali iliyozua dhana kuwa walikuwa kwenye ushindani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *