Gossip

Msanii Iyanii Afichua Bado Ni Bikira, Asema Atasubiri Ndoa

Msanii Iyanii Afichua Bado Ni Bikira, Asema Atasubiri Ndoa

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Iyanii, amefichua kuwa bado ni bikira na ameamua kuhifadhi ubikra wake hadi atakapoingia kwenye ndoa rasmi na mpenzi wake, Kemunto.

Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Alex Mwakideu, Iyanii amesema kuwa yeye na mpenzi wake wamekubaliana kuishi maisha ya kutojihusisha na ngono kabla ya ndoa.

Hitmaker huyo “Donjo Maber”, amesisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya maadili yake binafsi na pia ni ishara ya heshima kwa mpenzi wake.

Iyanii, ameongeza kuwa uamuzi huo pia ni njia ya kuweka msingi imara kwa maisha yake ya kifamilia.

Kauli ya msanii huyo imezua mjadala miongoni mwa mashabiki, wengine wakimsifia kwa ujasiri na msimamo wake, huku baadhi wakionesha mshangao kutokana na hadhi yake kama msanii maarufu wa burudani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *