LifeStyle

Msanii Kid Cudi Aoa Mpenzi Wake wa Muda Mrefu Nchini Ufaransa

Msanii Kid Cudi Aoa Mpenzi Wake wa Muda Mrefu Nchini Ufaransa

Msanii maarufu wa muziki wa Rap na muigizaji mashuhuri, Kid Cudi, ametangaza rasmi kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Lola Abecassis Sartore, ambaye sasa anafahamika kwa jina jipya la ndoa, Lola Mescudi.

Ndoa hiyo ya kifahari ilifungwa tarehe 28 Juni 2025 katika eneo la kifahari la Cap Estel, lililopo katika mji wa Èze, kusini mwa Ufaransa. Sherehe hiyo ilifanyika kwenye bustani ya kuvutia inayotazama moja kwa moja Bahari ya Mediterania, ikihudhuriwa na ndugu wa karibu, marafiki wa familia na wageni maalum kutoka tasnia ya burudani.

Kid Cudi, ambaye jina lake halisi ni Scott Mescudi, ameweka wazi furaha yake kupitia mitandao ya kijamii, akionesha picha chache kutoka katika tukio hilo la kipekee, huku mashabiki na watu maarufu wakimpongeza kwa hatua hiyo muhimu ya maisha.

Ndoa hii inakuja wakati ambapo Kid Cudi ameendelea kuimarika kitaaluma, akiwa na mafanikio makubwa katika muziki, uigizaji na hata ubunifu wa mitindo.