Entertainment

Msanii Maandy awachana Ma-Dejaay wa Kenya kwa uzembe

Msanii Maandy awachana Ma-Dejaay wa Kenya kwa uzembe

Msanii wa kike nchini Maandy amewatolea uvivu madejaay wa Kenya kwa kuwa na uzembe kwenye utendaji kazi wao wa kucheza nyimbo za wasaniii wa humu nchini.

Kupitia instastory yake amesema madejaay wamekuwa kizingiti wa kupeleka muziki Kenya kimataifa licha ya mchekeshaji Eric Omondi kujitoa mhanga kupigania tasnia ya muziki nchini kwa kushinikiza asilimia 75 za nyimbo za Kenya zipigwe kwenye vyombo vya habari.

Hitmaker huyo wa “We ni Wetu” amesema licha ya wasanii kuachia nyimbo mpya kila kuchao bila kupoa madejaay wamekuwa wakicheza nyimbo za zamani kwenye Playlists zao kiasi cha kupitwa na vituo vya radio ambavyo vimekuwa mstari wa mbele kucheza nyimbo mpya za wasanii tofauti na madj ambao wamekuwa wakilaza damu kwenye kazi zao.

Hata hivyo amemalizia kwa kusema kuwa madeejay watano ndio anawaheshimu kwa utendaji kazi wao nchini huku akiwataja wengine waliosalia kama mzigo kwenye kiwanda cha muziki kwa kuwa hawana uzalendo wa kushabikia muziki wa Kenya.

“I want to free Kenyan DJ’s from the same playlist so much great new music has been released over the past year !! Mko lazy sana sanaaa!!! I only like 5 DJ’s ,hao wengine apana!!! You are the biggest disconnect. Do better. Even radio bumps new music immediately its out.” Ameandika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *