Msanii wa Chief Godlove, anayefahamika kwa jina la Pipi jojo, ameangua kilio hadharani baada ya kugundua kwamba ataanza ziara yake ya vyombo vya habari nchini Kenya bila ushirika wa meneja wake huyo maarufu.
Kupitia video inayosambaa mtandaoni, Pipijojo ameonekana akibubujikwa na machozi huku Chief Godlove akimfariji na kumtia moyo kabla ya safari yake.
Katika ujumbe aliouchapisha kupitia ukurasa wake wa Instagram, Chief Godlove amesema kuwa binti yake Pipi Jojo amepata mwaliko wa kwenda kwenye media tour nchini Kenya, na kwamba alitarajia kumsindikiza mwenyewe lakini alishindwa kutokana na majukumu ya kikazi.
Ziara hiyo inatarajiwa kuanza wiki ijayo, ambapo Pipi jojo atazuru vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini Kenya kwa ajili ya kutangaza miradi yake mipya ya muziki.
Ziara ya Pipijojo nchini Kenya inatazamiwa kuwa hatua muhimu katika kukuza jina lake kimataifa na kuimarisha ushawishi wa muziki wa lebo ya Chief Godlove katika ukanda wa Afrika Mashariki.