
Msanii nyota nchini Exray Taniua anazidi kuchana mbuga kimataifa hii ni baada ya kutangaza ujio wa kolabo zake na wasanii nyota nchini Nigeria.
Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Exray amethibitisha kuwa ana kolabo mbili na simi pamoja Mr. Eazi ambapo amewataka mashabiki zake wampe ushauri ni kolabo gani kati ya wasanii hao aachie kwanza.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wamependekeza aachie kolabo zote mbili huku wengine wakimshauri aachia kola yake na Simi kwani moja kati ya wadada ambao muziki wao unawakosha.
Huu ni muundelezo mzuri kwa Exray ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akiachia nyimbo bila kupoa.