
Msanii wa Bongofleva TID ametangaza ujio wa album yake mpya ambayo ana mpango wa kuiachia ndani ya mwaka huu wa 2022.
Akizungumza na refresh TID amesema tayari album yake mpya imekamilika kwa asilimia mia moja na kilichobaki kwa sasa ni suala la kuiachia ila hajatuambia tarehe rasmi ya album hiyo kuingia sokoni.
Hitmaker huyo wa “Nyota Yangu” amesema album yake mpya itaitwa ni yeye huku akiwataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kuipokea album hiyo kwani amefanya na wasanii mbali mbali wa bongofleva.
Hii itakuwa ni album ya nane kutoka kwa mtu mzima TID baada ya mnyama na wanyama ya mwaka wa 2014.