
Mwanamuziki kutoka Kenya Willy Paul ameamua kutuonyesha jeuri za pesa anazozitolea jasho kupitia muziki wake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametusanua kuwa amenunua runinga ya inch 86 aina ya LG iliyomgharimu kiasi cha shillingi laki 5 za Kenya.
Bosi huyo wa Saldido amesema amechukua hatua hiyo kwa ajili ya kusherekea mafanikio ya wimbo wake mpya You aliyomshirikisha Guchi kutoka Nigeria.
Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii wa Kenya kuacha wivu ya mafanikio kwa wasanii wenzao na badala yake watie bidii kwenye kazi zao ili waweze kukithi mahitaji yao ya kimsingi ikiwemo kuvalia vizuri.
Willy Paul kwa sasa anafanya vizuri na single yake mpya You akiwa ameshirikisha Guchi kutoka Nigeria ambayo ina zaidi ya watazamaji laki 5 tangu iachiwe rasmi wiki kadhaa zilizopita.