
Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Yammi, amekanusha madai ya kununuliwa gari na lebo ya The African Princess, akieleza kuwa gari aliloonekana nalo lilikuwa la kukodisha. Hii ni baada ya msanii mwake wa zamani Nandy kuposti picha za gari hilo mtandaoni, hatua iliyowafanya mashabiki kuamini kuwa ni zawadi kutoka kwa lebo.
Mashabiki wengi walidhani kuwa lebo ya The African Princess imemnunuia Yammi gari jipya kutokana na mafanikio yake ya muziki, kwani hakukuwa na ufafanuzi wa moja kwa moja kutoka upande wa lebo baada ya tetesi kusambaa.
Hata hivyo, Yammi amesema lengo lake kwa sasa kama msanii huru ni kuwekeza nguvu kwenye kazi yake ya sanaa na kuendelea kuwapa mashabiki muziki bora. Kwa sasa anafanya vizuri na EP yake mpya iitwayo After All, ambayo imebeba jumla ya nyimbo sita kali za moto, ikiwa na collabo moja pekee.
Kupitia kazi hiyo mpya, Yammi ameendelea kuthibitisha nafasi yake katika tasnia ya muziki wa Bongofleva, akipata mapokezi makubwa kutoka kwa mashabiki ndani na nje ya Tanzania.