Entertainment

MSANIII BANDANAH MIQASAH ATANGAZA KUREJEA RASMI KWENYE MUZIKI

MSANIII BANDANAH MIQASAH ATANGAZA KUREJEA RASMI KWENYE MUZIKI

Mwanamuziki Bandanah Miqasah ametangaza kurejea rasmi kwenye game ya muziki nchini baada ya ukimya wa miaka miwili.

Bandanah amethibitisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Bandanah ambapo amewataka mashabiki zake wakae mkao wa kula kupokea ujio wake mpya ambao ameutaja ni wa kitofauti sana kwani ana mpango wa kuachia ngoma mfululizo bila kupoa.

Msanii huyo amedokeza kuachia wimbo mpya uitwao Pate/Birthday, Aprili 7 mwaka huu, wimbo ambao umetayarishwa chini ya uongozi wa Cash Group Entertainment lebo inayomilikiwa na msanii Krg The Don.

“ITS BEEN 2 YEARS NOW SINCE I WENT OFF THE GAME (silent/missing) GET READY FOR MY BACK TO BACK COME BACK IN THE KENYAN MUSIC SCENE OFFICIALLY FROM THIS 7th of APRIL (@bandanahmiqassa and @vdj_jones ~ DROPPING (PATE / BIRTHDAY) THIS THURDSAY at EXACTLY 10:00am Audio Prd By @daviproducer Video Dir by @steveblackson Special Thanks To @krgthedon and The Entire Team of @superstar_ent_ke and @fastcashmusicgroup Lets Take Over The Game 🔥🔥🔥🔥🔥 2022 BACK TO THE BASICS #projectx

#ramadankareem and #happyfasting #saummaqbul MNIPOKEE KWA UWEZO WA ALLAH ❤️🙏❤️,” Ameandika kupitia Instagram.

Utakumbuka Bandanah alipata umaarufu nchini miaka  minne iliyopita kupitia ngoma iitwayo Kidege aliyomshirikisha Naiboi pamoja na Spizzo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *