Klabu ya Barcelona imekamilisha usajili wa Mshambuliaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu akitokea Arsenal kama mchezaji huru.
Kabla yakuondoka Gunners Aubameyang hakuwa akipata nafasi ya kucheza mbele ya kikosi cha Arteta kufuatia kutajwa kua mtovu wa nidhamu
Aubameyang amewaaga rasmi mashabiki na wapenzi wa klabu ya Arsenal, kufuatia makubaliano ya pande zote kuondoka katika klabuni hapo.
“Kuwa na nafasi ya kushinda mataji na heshima ya kuwa nahodha wa klabu hii ni jambo nitaliweka moyoni mwangu milele”.