Entertainment

Mtoto Aonyesha Upendo kwa Muziki wa Toxic Lyrikali kwa Kuchana “Long Story” Bila Kukwama

Mtoto Aonyesha Upendo kwa Muziki wa Toxic Lyrikali kwa Kuchana “Long Story” Bila Kukwama

Shabiki mdogo wa muziki ameibua mshangao na furaha mitandaoni baada ya kuonyesha kipaji chake cha kipekee kwa kuuchana wimbo maarufu wa rapa Toxic Lyrikali, Long Story, bila kukosea hata mstari.

Clip ya video inayomuonyesha mtoto huyo ikisindikiza mashairi ya wimbo huo kwa ustadi mkubwa imeenea kwa kasi, jambo lililowagusa mashabiki wengi wa hip hop na kumfanya avune sifa tele.

Mashabiki wengi wamepongeza hatua ya mtoto huyo, wakisema ni ishara ya namna muziki wa Toxic Lyrikali unavyowagusa hata vijana wadogo. Baadhi wamesema kitendo hicho kinadhihirisha jinsi muziki unaweza kuvuka vizuizi vya umri na kuwa chombo cha kuunganisha watu.

Wimbo Long Story, uliotolewa miezi sita iliyopita, umeendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa ya kidigitali ukiwa na zaidi ya watazamaji milioni moja kwenye YouTube. Toxic Lyrikali, ambaye amejizolea mashabiki kutokana na uandishi wake wa kina na uwasilishaji wa hisia halisi, amekuwa akitambulika kama mmoja wa wakali wa rapa wa kizazi kipya nchini Kenya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *