Gossip

Mulamwah Aingilia Sakata la Ruth K na Mfanyikazi wake

Mulamwah Aingilia Sakata la Ruth K na Mfanyikazi wake

Mchekeshaji kutoka Kenya, Mulamwah, amefunguka kuhusu sakata linaloendelea mitandaoni kati ya Baby Mama wake Ruth K na aliyekuwa mfanyikazi wake Ann Waithera ambapo inadaiwa mtoto wake alitumika kutengeneza maudhui mtandaoni.

Kupitia Instagram, Mulamwah amesema kuwa mwanawe hapaswi kuingizwa kwenye drama za watu wazima.Amewaonya Baby Mama wake na mfanyikazi wake kuacha kabisa kumtumia mtoto wake kama chanzo cha kutengeneza maudhui mtandaoni.

Kauli hiyo ya Mulamwah imekuja wakati ambapo mgogoro mkali unaendelea kati ya baby mama wake Ruth K na aliyekuwa mjakazi Ann Waithera. Ruth K alidai Ann aliiba iPhone 14 yake na kudukua akaunti za Instagram na TikTok za mtoto wake, jambo lililozua mjadala mkubwa mtandaoni.

Kwa upande wake, Ann Waithera amekanusha madai hayo akisema kuwa hayana msingi wowote. Badala yake, amemgeukia Ruth K akimtuhumu kutumia mtoto wake kama content ili kuvuta hisia za Mulamwah baada ya kurudiana na baby mama wake wa kwanza Carrol Sonnie.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *