Gossip

Mulamwah na Carol Sonnie Wazidisha Tetesi za Kurudiana

Mulamwah na Carol Sonnie Wazidisha Tetesi za Kurudiana

Mchekeshaji na mbunifu wa maudhui nchini Kenya, Mulamwah, pamoja na baby mama wake Carol Sonnie, wamezua gumzo mitandaoni baada ya wawili hao kushare picha wakionekana kuwa kwenye date maalum ya kifamilia wakiwa pamoja na mtoto wao.

Kupitia picha na video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Mulamwah na Carol Sonnie walionekana wakifurahia muda pamoja, jambo lililowafanya mashabiki wengi kuanza kuhisi huenda wawili hao wameamua kurejesha uhusiano wao kwa siri.

Hata hivyo, wawili hao wamesisitiza kuwa kukutana kwao kulilenga kumpa mtoto wao upendo wa baba na mama, wakieleza kuwa walifanya hivyo kwa maslahi ya mtoto wao na si kwa nia ya kurudiana kimapenzi.

Licha ya ufafanuzi huo, mashabiki wameendelea kuhoji ukweli wa kauli hiyo, wakidai ukaribu na mazingira ya date hiyo yanaashiria zaidi ya malezi ya mtoto pekee. Tetesi hizi zimezidi kupata uzito hasa ikizingatiwa kuwa Mulamwah aliachana na baby mama wake mwingine, Ruth K, miezi kadhaa iliyopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *