Entertainment

MUME WA NICK MINAJ AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 JELA

MUME WA NICK MINAJ AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 3 JELA

Mume wa Nicki Minaj, Kenneth Petty amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu chini ya Uangalizi wa Mahakama pamoja na Kifungo cha nyumbani mwaka mmoja baada ya kukiri kushindwa kujisajili kama mkosaji wa Kingono (Sex Offender) katika Jimbo la California mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Mwanasheria wa Serikali, Mahakama pia imemtaka alipe faini ya dollar ($55,000).

Petty mwenye umri wa miaka 44, alihitajika kujisajili kama mkosaji wa Kingono baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka msichana wa miaka 16 mwaka 1995 ambapo alikaa Jela miaka 4.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *