Entertainment

MUME WA ZAMANI WA BRITNEY SPEARS ASHTAKIWA KWA KUZUA VURUGU

MUME WA ZAMANI WA BRITNEY SPEARS ASHTAKIWA KWA KUZUA VURUGU

Mume wa zamani wa mwanamuziki Britney Spears ameshtakiwa kwa kosa la kujitokeza bila taarifa wala kualikwa wakati wa harusi ya nyota huyo na Sam Asghari ambaye ni mume wake kwa sasa baada ya kufunga harusi.

Jason Alexander, mwenye umri wa miaka 40, alikana shtaka hilo, pamoja na kuingia bila kibali, kutumia nguvu na kuharibu mali.

Alikamatwa wiki iliyopita baada ya kudaiwa kugonga geti na kutoa video kutoka ndani ya nyumba ya Spears.

Bwana Alexander alimuoa Britney Spears ambaye alikuwa rafiki wa utotoni mwaka wa 2004 lakini ndoa yao ilidumu kwa kipindi cha chini ya siku tatu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *