Entertainment

MUONEKANO MPYA WA MAGIX ENGA WAZUA GUMZO MTANDAONI.

MUONEKANO MPYA WA MAGIX ENGA WAZUA GUMZO MTANDAONI.

Mionekano kwa wasanii si jambo la kuchukulia poa, bali ni kazi. Ni moja ya njia za branding na kujiweka machoni kwa mashabiki muda wote.

Sasa Prodyuza wa muziki nchini Magix Enga ameamua kuzinyoa nywele zake zote aina dread kichwani mwake (Kipara).

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Magix Enga amechapisha video akiwa amenyoa nywele hizo na kusindikiza caption inayosomeka, “Kichwa safi kama balloon”.

Prodyuzo huyo ambaye pia ni mwimbaji hajaweka wazi sababu za kuchukua maamuzi ya kuonyoa dread zake ila ameibua hisia mseto miongoni mashabiki zake pamoja na mastaa wenzake ambao walibaki na masuala ni kitu gani kilimpelekea kuchukua maamuzi hayo magumu.

“Kuriathiatia mutwe?” kwa maana ya “Nini mbaya na kichwa chako?” msanii Odi wa Muarang’a aliuliza.

Hata hivyo wasanii wengine kama Exray wamesema kuwa wana heshimu maamuzi yake huku wengine kama Bien wa Sauti Sol wakimpongeza kwa hatua kubwa aliyochukua.

Kwa muonekano wake mpya wa Magix Enga imeonyesha ni jinsi gani amebadilika kwa kuwa muonekano wake huyo umezua hisia mseto miongoni mwa mashabiki zake ambao wameandika ujumbe unaosomeka “looking different but cute … uko tu fiti new beginning ,looking marvelous”

“Hii stunt nayo imeeza. Hizo nywele sio zako. I know this is a scum”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *