LifeStyle

Muonekano Mpya wa Upara wa Harmonize Wazua Mjadala

Muonekano Mpya wa Upara wa Harmonize Wazua Mjadala

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Harmonize, ameibua gumzo mitandaoni baada ya kufichua muonekano wake mpya wa upara muda mfupi tu baada ya kuwasili nchini Kenya kwa shughuli zake za kimuziki.

Picha zake zikimuonyesha akiwa na mtindo huo mpya zilisambaa kwa kasi, na mashabiki wengi wameanza kutoa maoni mseto kuhusu hatua hiyo ya ghafla. Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamemkosoa wakidai kuwa muonekano huo unafanana sana na ule wa msanii nyota wa Nigeria, Asake, wakisema Harmonize ameiga mtindo huo wa upara ili kuendana na mwelekeo wa wasanii wa Afrika Magharibi.

Hata hivyo, wapo mashabiki wengine waliomtetea, wakisema msanii ana haki ya kubadilisha mwonekano wake kadri anavyojisikia na kwamba ubunifu wa wasanii haupaswi kufungwa na maoni ya watu.

Muonekano huo mpya umeongeza msisimko kuhusu ziara yake ya Kenya, huku wengine wakisubiri kuona kama ni sehemu ya maandalizi ya Albamu yake mpya iitwayo 31 au ni mabadiliko ya kawaida ya mtindo wa maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *