Gossip

Vera Sidika Afichua Kufanyiwa Upasuaji wa Kupunguza Makalio

Vera Sidika Afichua Kufanyiwa Upasuaji wa Kupunguza Makalio

Mrembo maarufu na mjasiriamali wa mitandaoni, Vera Sidika, amezua gumzo mitandaoni baada ya kufichua kuwa alifanyiwa upasuaji wa kupunguza makalio kutokana na matatizo ya kiafya aliyoyapata kufuatia mabadiliko ya awali ya mwili wake.

Kupitia ujumbe aliouandika kwenye Instagram, Vera amesema alilazimika kupitia hatua hiyo baada ya kupitia kipindi kigumu sana kiafya, hali iliyomlazimu kufanya maamuzi ya kubadili muonekano wake kwa mara nyingine. Mama huyo wa mtoto mmoja ameongeza kuwa safari hiyo haikuwa rahisi, na imeacha athari kubwa katika maisha yake.

Vera amewashauri wanawake kujikubali jinsi walivyo na kutokubali kushawishiwa na shinikizo la mitindo au marafiki kuingia kwenye upasuaji wa kubadilisha miili yao. Amesisitiza kuwa hatua kama hizo zinaweza kuwa na madhara ya muda mrefu kiafya na kiakili.

“Wanadada tafadhalini, mjue kujipenda mlivyo na msikubali shinikizo la rika liwafanye mkimbilie kufanya mambo ambayo yatawaharibia maisha yenu huko mbeleni,” aliandika Instagram

Haya yanajiri miaka kadhaa baada ya Vera kuwa gumzo kwa mara nyingine kwa kuonekana akiwa na muonekano tofauti wa ngozi, ambapo alidai kuwa ameachana na bidhaa za kubadilisha rangi ya ngozi. Hata hivyo, madai hayo baadaye yalitafsiriwa na wengi kuwa yalikuwa mbinu ya kiki kwa ajili ya kutangaza mradi mpya.

Vera Sidika, ambaye ni miongoni mwa watu maarufu wenye ushawishi mkubwa mitandaoni nchini Kenya, ameonekana kuchukua mwelekeo mpya wa maisha kwa kutoa tahadhari na elimu kwa mashabiki wake, hasa wanawake, kuhusu hatari za kubadilisha maumbile kwa njia za upasuaji.