Gossip

Muonekano mpya wa Vivian wazua gumzo

Muonekano mpya wa Vivian wazua gumzo

Mwanamuziki Vivian ametuonyesha muonekano wake mpya baada ya kuzinyoa nywele zote kichwani (Kipara).

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa ameamua kuja na muonekano wa kitofauti kama njia ya kukumbatia ukurasa mpya wa maisha yake siku chache baada ya kuthibitisha kupitia wakati mgumu mahusiano yake na mume wake Sam West yalipoingiwa na ukungu.

Muonekano wa sasa umeonekana kuteka mazungumzo zaidi mtandaoni, huku baadhi wakidai kuwa huenda mrembo huyo ana kazi mpya ambayo ataiachia hivi karibuni.

Mionekano kwa wasanii si jambo la kuchukulia poa, bali ni kazi. Ni moja ya njia za branding na kujiweka machoni kwa mashabiki muda wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *