
Aliyekuwa meneja wa Sailors Gang Mwalimu Rachael amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya msanii Cocos Juma kumtuhumu kuwa alipora shillingi millioni 15 za kundi hilo.
Kupitia chaneli yake ya Youtube Mwalimu Rachael amesema ameshangazwa na kitendo cha Cocos Juma kumzushia taarifa za uongo kuwa aliwatapeli pesa zao ikizingatiwa kipindi anasimamia muziki  wao alihakikisha kila msanii wa kundi hilo anafaidi na mirahaba ya nyimbo zao.
Aidha ameenda mbali zaidi na kusema kwamba masaibu yanayowaandama wasanii wa Sailors Gang yametokana na wao kumpuuza alipowakataza kujiunga na lebo ya Black Markert Records ambayo imesambaratisha kimuziki.
Mwalimu rachael amefichua kwamba wasanii hao wamekuwa wakijaribu kumuomba msamaha arudi afanye nao kazi lakini amekataa ombi lao kutokana na wao kumharibia brand yake kwa kumzushia taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo amedokeza mpango wa kuwatambulisha wasanii wake wapya chini lebo yake ya muziki ya MRX Media licha ya wasanii wa Sailors kumharibia jina na hata kumkatisha tamaa kwenye suala la kuwasimamia wasanii.