Gossip

Mwanablogu Eve Mungai Aapa Kuwaanika Wanaume Wanaomtumia Picha Chafu

Mwanablogu Eve Mungai Aapa Kuwaanika Wanaume Wanaomtumia Picha Chafu

Mwanablogu na mshawishi maarufu wa mitandao ya kijamii nchini Kenya, Eve Mungai, ameapa kuchukua hatua kali dhidi ya wanaume walio katika ndoa wanaomtumia picha zisizofaa kupitia jumbe za moja kwa moja (DMs) kwenye mitandao yake ya kijamii.

Kupitia chapisho kali kwenye Instagram Stories, Eve alionyesha kuchoshwa na tabia ya baadhi ya wanaume waliooa kumtumia maudhui ya matusi na picha za ngono, akisema kuwa wakati umefika wa kuanika majina yao hadharani.

“Wanaume waliooa, mna wake zenu halafu bado mnanitumia picha za ajabu kwenye DM? Msidhani mtatulia! Saa imefika ya kuwaanika,” aliandika Eve kwa hasira.

Eve Mungai, ambaye amejijengea jina kwa maudhui ya kijamii na mahojiano ya kuvutia na watu mashuhuri, aliongeza kuwa vitendo hivyo si tu vya kukosa heshima bali pia vinadhalilisha wake wa wanaume hao. Alisema kuwa wanawake wengi hawajui wanachoendelea nyuma ya pazia, na kama njia ya kupambana na tabia hizo, ataanza kuwataja wahusika kwa majina.

Kauli yake imezua mjadala mkali mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakimpongeza kwa kusimama kidete kupinga udhalilishaji wa kingono, huku wengine wakimtaka kuwa na subira na kushughulikia suala hilo kwa njia ya binafsi.