Gossip

Mwanamume Amuanika Akothee Mtandaoni kwa Kosa la Kutolipa Deni la Miezi Mitano

Mwanamume Amuanika Akothee Mtandaoni kwa Kosa la Kutolipa Deni la Miezi Mitano

Msanii maarufu wa Kenya, Akothee, amejikuta katika hali ya lawama baada ya mwanamume mmoja kujitokeza hadharani akimshutumu kwa kutolipa deni linalodaiwa kudumu kwa zaidi ya miezi mitano.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwanamume huyo anadai kuwa alifanya kazi ya design na kurekebisha reception ya ofisi ya Akothee, akajitahidi kufanya kila aliloagizwa, hata kurekebisha makosa yaliyotokea wakati wa utekelezaji wa majukumu yake.

 “Akothee nilikufanyia kazi. Saa hii ni miezi mitano. Kazi nilifanya, reception nilifanya, ukatoa makosa nikarekebisha,” alisema kwa masikitiko.

Anadai kuwa baada ya kumaliza kazi hizo, Akothee alizima simu yake, akamzuia kwenye WhatsApp, na hata hakuwahi kujibu ujumbe wowote wala kupokea simu zake. Pia alifichua kuwa licha ya matatizo ya kifedha anayopitia, bado analazimika kulipa baadhi ya gharama alizotumia wakati wa kazi, ikiwemo gari aliloleta hadi kwenye ofisi ya msanii huyo.

 “Bado kuna vitu nafaa kulipa. Ile gari ilinileta mpaka kwa ofisi yako, hiyo gari nafaa kulipa. Tafadhali tu, naomba nilipe,” aliongeza kwa sauti ya unyonge.

Mwanamume huyo alisisitiza kuwa hana nia mbaya na Akothee, wala hajitafutii umaarufu kupitia mgogoro huo, bali analilia haki yake kama mfanyakazi.

Mpaka sasa, Akothee hajatoa kauli rasmi kuhusu tuhuma hizo, lakini mashabiki na wafuasi wake kwenye mitandao wamegawanyika, baadhi wakimtetea na wengine wakitaka atoe maelezo au kumlipa mwanaume huyo ikiwa madai ni ya kweli. Hata hivyo, tukio hilo limezua mjadala mitandaoni kuhusu haki za wafanyakazi na uwajibikaji wa watu maarufu katika kulipa huduma wanazopewa.