Entertainment

Mwanamuziki kutoka Uganda Vinka atangaza ujio mpya 2023

Mwanamuziki kutoka Uganda Vinka atangaza ujio mpya 2023

Msanii kutoka nchini Uganda Vinka ametangaza ujio wa album mpya mwaka wa 2023 ikiwa ni miaka tatu zimepita tangu awabariki mashabiki zake na album iitwayo Love Doctor iliyotoka mwaka 2019

Vinka ambaye amekuwa kwenye muziki kwa takriban miaka sita amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kupokea album yake mpya ambayo kwa sasa anaifanyia kazi.

Aidha Hitmaker huyo wa Thank God amesema kwa sasa hana mpango wa kuja na tamasha lake la muziki kama namna wasanii wengine nchini uganda wanavyofanya ikizingatiwa kuwa ana majukumu ambayo anayashughulikia kwenye muziki wake.

Lebo ya Swangz Avenue kwa mwaka huu pekee imefanya matamashs mawili makubwa kwa wasanii wake Azawi na Winnie Nwagi ambao walijunga na lebo hiyo mwaka wa 2019 baada ya Vinka.

Hata hivyo tetesi za ndani kutoka kwa watu wa karibu na vinka zinadai kuwa huenda mrembo huyo akaanda tamasha lake la muziki mwaka ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *