Entertainment

Mwanamuziki wa Canada Paa Kwaci mbioni kuachia wimbo mpya

Mwanamuziki wa Canada Paa Kwaci mbioni kuachia wimbo mpya

Msanii wa Hiphop kutoka nchini Canada Paa Kwaci amefichua mpango wa kuachia wimbo mwingine baada ya wimbo wake Mama Africa kuendelea kufanya vizuri kwenye majukwaa yote ya kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook Paa Kwaci amesema tayari ameingia studio kwa ajili ya kuurekodi wimbo huo ambao ameupa jina la Pushin Me

“Recording a new song called “Pushin Me.”, Aliandika.

Licha ya kutoweka wazi ni lini wimbo utaingia sokoni, rapa huyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea wimbo huo ambao ameutaja kuwa wa kitofauti.

Kauli yake hiyo imekuja siku chache mara baada ya kuweka wazi jina la wimbo wake na staa wa muziki kutoka Marekani Sean Kingston, Baba Remix huku pia akidokeza ngoma nyingine iitwayo Bragging Rights atakayomshirikisha rapa mkongwe duniani Snoop Dog na Khatun Snow.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *