
Mwimbaji wa nyimbo za Soul nchini Kenya Muthaka ameshinda tuzo ya Kimataifa inayofanyika Afrika kila mwaka maarufu kama AFRIMA.
Katika tuzo hizo zilizofanyika Jijini Dakar nchini Senegal siku ya Jumapili ya tarehe 15 Januari 2023 Muthaka amefanikiwa kushinda tuzo hiyo katika kipengele cha “Best Female Artiste in East Africa” ambapo amewashukuru mashabiki zake kumpigia kura.
“Thank you @afrima.official 🙏 Not me thanking my dog 💀 I’d be lying if I said I even remember what I was saying but this moment isn’t something I can properly articulate.”
“I would like to share this with all the Kenyan artists, and especially all Female artists who write their own music. It’s incredibly important to express what is in your mind and share what is in your heart even if its different from what everyone else is doing, what you have to give matters and no one can say it better than you can for yourself ❤”, Aliandika.
Muthaka anakuwa ni mwimbaji wa pekee kutoka Kenya kushinda tuzo hiyo na kuweka alama ya kukumbukwa katika Tasnia ya Muziki wa nchini humo.