Entertainment

MWANAMUZIKI WA UGANDA VIVIAN TENDO ADAI MAISHA YAKE YAMO HATARINI

MWANAMUZIKI WA UGANDA VIVIAN TENDO ADAI MAISHA YAKE YAMO HATARINI

Mwanamuziki wa kike kutoka nchini uganda Vivian Tendo amefunguka na kudai kuwa maisha yake yamo hatarini.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram mrembo huyo ameshare audio clip ya meneja wake wa zamani Oman rafiki akimtolea vitisho na kuweka wazi kuwa anaishi kwa hofu kwani huenda meneja wake huyo akamuangamiza.

Hitmaker huyo wa “Timango” amesema amejaribu kunyamazia suala hilo kwa muda na hata kukwepa interviews mbali mbali ili asizungumzie vibaya uongozi wake wa zamani lakini maji yamezidi unga kwa upande wake ambapo amewataka mashabiki na wanafamilia wake kumuwajibisha Oman Rafiki ikitokea amefariki ghafla.

Kauli ya mrembo huyo inakuja siku chache baada ya Oman Rafiki kunukuliwa kwenye moja ya interviews akisema kuwa ana mpango wa kumfungulia mashtaka viviam tendo kwa madai ya kukiuka mkataba wake na lebo ya Route Entertainment.

Utakumbuka Vivian Tendo aliachana na uongozi wake wa Route Entertainment mwezi disemba mwaka wa 2021 kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi lakini inaonekana meneja wake wa zamani Oman Rafiki hataki kumuacha mrembo huyo salama kwani amewekeza pesa zake nyingi kwenye muziki wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *