Entertainment

Mwanariadha Usain Bolt atapeliwa mabillioni ya pesa kwenye akaunti yake

Mwanariadha Usain Bolt atapeliwa mabillioni ya pesa kwenye akaunti yake

Mwanariadha anayeshikilia rekodi za dunia katika mbio za mita 100 na mita 200, Usain Bolt kutoka Jamaica anaripotiwa kupoteza mabilioni ya pesa kupitia ulaghai mkubwa.

Kulingana na jarida la AFP, mamlaka inayosimamia fedha nchini Jamaica imeanzisha uchunguzi dhidi ya kampuni ya kuwekeza pesa ambayo Bolt alikuwa amewekeza pesa zake na ambazo zimeofiwa kutoweka kwa njia za ulaghai.

Meneja wa Bolt Nugent Walker aliliambia gazeti la Jamaica Gleaner kwamba mwanariadha huyo aliyestaafu, amekuwa na uwekezaji na kampuni hiyo kwa zaidi ya muongo mmoja. “Hatua zote muhimu zimechukuliwa ili kufafanua jambo hili.” Walker aliambia jarida hilo, akisema mwanariadha huyo aligundua hitilafu kwenye akaunti yake siku ya Jumatano.

Kwa mujibu wa taarifa toka kwenye mitandao ya nchini Jamaica ukiwemo Jamaica Observer, umeripoti kwamba Bolt amepoteza kiasi cha zaidi ya KSh. Bilioni moja. Kwa sasa akaunti yake inasoma takribani KSh. Elfu 248,200.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *