Entertainment

MWANASHERIA WA KESI YA UBAKAJI INAYOMKABILI CHRIS BROWN AJITOA

MWANASHERIA WA KESI YA UBAKAJI INAYOMKABILI CHRIS BROWN AJITOA

Mwanasheria wa kesi ya ubakaji ambayo inamkabili Chris Brown ametangaza kujitoa kwenye shauri hilo.

Ariel Mitchell amesema amejitoa kufuatia ushahidi wa sauti (voice note) pamoja na ujumbe mfupi ambazo chris brown alizianika hadharani zikionesha hakuwa na hatia.

Ushahidi uliotolewa na Breezy ulimuanika wazi mwanamke huyo kuwa ndiye alikuwa akimuhitaji mwimbaji huyo wa R&B tofauti na madai yake.

Mwanasheria huyo amesema mteja wake hakumueleza ukweli kabla ya kumfungulia mashtaka Chris brown kwani angefuta kesi dhidi ya msanii huyo.

Chris Brown ameendelea kudai aombwe msamaha hadharani, lakini pia ameendelea kuvitaka vyombo habari kuripoti habari hii kama ambavyo waliripoti tuhuma zake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *