Gossip

Mwanaume wa Kenya Afichua Alimdanganya Mkewe kwa Mwaka Akijifanya Eric Omondi

Mwanaume wa Kenya Afichua Alimdanganya Mkewe kwa Mwaka Akijifanya Eric Omondi

Mwanaume mwenye sura inayofanana na mchekeshaji wa Kenya, Eric Omondi, amekiri kuwa aliishi katika uhusiano wa kimapenzi kwa mwaka mmoja akijifanya kuwa yeye ndiye mchekeshaji huyo halisi.

Kwa mujibu wa mahojiano yaliyosambaa mtandaoni, amesema kuwa alikutana na mwanamke huyo mtandaoni na wakaanza mahusiano, huku akitumia umaarufu wa Eric Omondi kumvutia na kumfanya aamini kuwa anachumbiana na staa huyo.

Mwanaume huyo amesema kwa muda wa mwaka mmoja, alidumisha uongo huo kwa kutumia picha na video za Eric Omondi mitandaoni, jambo lililomfanya mwanamke huyo asiwe na shaka. Baada ya muda, ukweli ulifichuka na mpenzi wake kugundua kuwa alikuwa akiishi na mtu tofauti kabisa.

Mwanaume huyo amekiri kosa hilo akisema kuwa hakupanga kumuumiza mwanamke huyo, bali alijikuta akizama zaidi katika uongo huo kutokana na hofu ya kumpoteza. Amesema alianza kama mzaha, lakini baadaye mambo yakachukua mwelekeo tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *