Entertainment

Mwanaume wa makamu atishia kujitoa uhai kisa kuibiwa mpenzi na Willy Paul

Mwanaume wa makamu atishia kujitoa uhai kisa kuibiwa mpenzi na Willy Paul

Baada ya msala wa video ya wimbo wa “Lalala” kufutwa Youtube kwa madai ya hakimiliki na kisha kurejeshwa, sasa ni zamu ya mwanaume mmoja ambaye amejitokeza na kutishia kujitoa uhai kutokana na hatua ya Willy Paul kumnyang’anya mpenzi wake Jovial.

Kwa mujibu wa video inayosambaa mtandaoni, mwanaume huyo anadai Jovial ni mpenzi wake wa muda mrefu ambapo ameenda mbali zaidi na kusisitiza kuwa wamebarikiwa kupata mtoto wa pamoja.

Kauli ya mwanaume huyo imeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonekana kuzipuzilia mbali tetesi hizo wakidai ni kiki huku wengine wakiwa wamebaki na mashangao kwa kitendo cha mwanaume huyo kuangua kilio hadharani kisa mapenzi.

Hata hivyo Willy Paul amepuzilia mbali tuhuma hizo kwa kusema kwamba  hazina ukweli wowote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *