
Mwigizaji maarufu nchini Marekani Terrence Howard amefanya mahojiano na Podcast ya PBD na kumwaga sumu kali kuhusu rapa Diddy. Kwa mujibu wa Terrence Howard, anasema Diddy alitaka kumuingilia kimwili. Hii ni baada ya mwigizaji huyo kualikwa nyumbani kwa rapa huyo kwa lengo kumfundisha uigizaji kama ambavyo ombi lake lilikuwa linasema.
Baada ya kufika, Terrence anasema alianza kuzungunza na Diddy lakini macho yake yalikuwa yakimtazama sana kiasi cha kugundua kwamba hakuna usalama mahali pale. Baadaye msaidizi wa Terrence ikabidi amchane boss wake kwamba, Diddy anataka kutoka na wewe wiki ijayo, na anataka kukuingilia kimwili.
Aidha muigizaji huyo mkongwe amesema, vijana wengi wamekuwa wakiangukia kwenye mtego huo kwa sababu ya kutaka kufanikiwa kwenye vitu wanavyopenda.