Gossip

Mwijaku Akanusha Madai ya Kukosa Makazi kwa Kutamba na Mali zake

Mwijaku Akanusha Madai ya Kukosa Makazi kwa Kutamba na Mali zake

Mtangazaji na mdau wa burudani, Mwijaku, amejigamba waziwazi kuhusu mali anazodai kumiliki, huku akimshambulia vikali msanii mkongwe Dudu Baya kwa madai ya kukosa makazi na maisha ya uhakika.

Akizungumza kupitia moja ya mitandao ya kijamii, Mwijaku ametamba kuwa ana nyumba yake binafsi, magari pamoja na runinga kubwa ya inchi 100 huku akisisitiza kuwa mafanikio hayo yametokana na juhudi na kazi yake binafsi.

Mwijaku hakusita kumrushia Dudu Baya maneno mazito, amedai kuwa msanii huyo anaishi kwenye baa na hana maisha aliyoyapanga. Ameongeza kuwa Dudu Baya amekuwa akiombaomba watu wamchangie na kumkopesha kodi ya nyumba.

Kwa mujibu wa Mwijaku, mafanikio hayo yanamtofautisha pakubwa na Dudu Baya ambaye amedai hana maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *