Gossip

Mwijaku Akubali Kuzichapa na Dudu Baya

Mwijaku Akubali Kuzichapa na Dudu Baya

Mtangazaji na mdau wa burudani, Mwijaku ameonekana kuumizwa na tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake na msanii mkongwe Dudu Baya ambapo amekiri hadharani yuko tayari kuzichapa naye ana kwa ana iwapo itaendelea kuvuka mipaka ya kumvunjia heshima.

Akizungumza kwa hasira, Mwijaku amesema amechoshwa na kile alichokitaja kuwa ni tuhuma za uongo na za kumdhalilisha, akidai Dudu Baya hana uwezo wa kumshinda kwa hali yoyote iwe kifedha, kiuchawi wala kiunguvu.

Mwijaku amekanusha vikali madai yaliyotolewa na Dudu Baya kuwa hana makazi na kwamba aliwahi kuwa shoga wakati wa masomo yake chuoni, akisisitiza kuwa taarifa hizo hazina msingi wowote na zinalenga kumharibia jina.

Hata hivyo, Mwijaku ameonya kuwa hatamvumilia tena Dudu Baya endapo ataendelea kumvunjia heshima kwa kumzushia taarifa za uongo, akisema yuko tayari kuchukua hatua kali ili kulinda jina na heshima yake mbele ya umma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *