Mtangazaji na mdau wa burudani, Mwijaku, amemlaumu staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kwa kudai kuwa ndiye chanzo cha kuvunjika kwa ndoa yake.
Akizungumza kupitia mitandao ya kijamii, Mwijaku amesema kuwa tangu aanze kuwa karibu na Diamond, maisha yake ya ndoa yalianza kuyumba na hatimaye kusambaratika. Amedai kuwa ukaribu wake na Diamond ulimuingiza kwenye mtindo wa maisha uliosababisha migogoro ya mara kwa mara ndani ya ndoa yake.
Kwa mujibu wa Mwijaku, mazingira na mienendo inayomzunguka Diamond si rafiki kwa watu wenye ndoa au mahusiano ya kudumu, akidai kuwa kuna ushawishi unaovuruga misingi ya familia kwa wale wanaokuwa karibu naye.
Hata hivyo Mwijaku, amempa onyo msanii Jux, akimtaka ajitengenezee mipaka na kujitenga na Diamond mapema kabla mambo hayajaharibika katika ndoa yake. Amesisitiza kuwa ushauri huo unatokana na uzoefu wake binafsi na alichokipitia.