Gossip

Mwijaku Amlilia Mke Wake Amrudie Baada ya Kuguswa na Uchumba wa Harmonize na Kajala

Mwijaku Amlilia Mke Wake Amrudie Baada ya Kuguswa na Uchumba wa Harmonize na Kajala

Mtangazaji na mdau wa burudani kutoka Tanzania, Mwijaku, amegusa hisia za mashabiki zake baada ya kumlilia mke wake hadharani kupitia mitandao ya kijamii, akimuomba arejee katika maisha yake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mwijaku alishiriki video ya wasanii Harmonize na Kajala Masanja wakifurahia maisha mara baada ya kuvishana pete ya uchumba. Video hiyo ilionekana kumgusa moja kwa moja, hali iliyomfanya kutoa ujumbe mzito uliojaa hisia.

Katika ujumbe huo, Mwijaku amemwomba mke wake amrudie, akieleza kuwa hawezi kuendelea na maisha bila uwepo wake. Ameongeza kuwa anatamani kurejea katika maisha ya ndoa na kufurahia furaha ya familia kama alivyoshuhudia kwa Harmonize na Kajala.

Hatua ya Mwijaku imeonyesha wazi maumivu na hamu ya kutaka mke wake amrudie baada ya kumkimbia kutokana na madai ya usaliti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *