Entertainment

Mwimbaji wa Injili nchini Tanzania Flora Mbasha abadili jina la Usanii

Mwimbaji wa Injili nchini Tanzania Flora Mbasha abadili jina la Usanii

Mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania aliyejulikana kwa jina ya Flora Mbasha ametangaza ujio wake mpya ambapo atakuwa chini ya menejimenti nyingine.

Akizungamza na waandishi wa habari Jijini Mwanza Dada Flora Mayala amesema baada ya ukimya wa muda mrefu amerejea akiwa na nyimbo nzuri zenye kuijenga jamii kumjua Mungu ambapo pia amemtambulisha Meneja wake mpya ambaye ni Ezekiel Moleli.

Kwa upande wake Ezekiel Moleli amesema kwa sasa jina la Flora Mbasha halitotumika ambapo jina analotumia muimbaji huyo ni Dada Flora Mayala huku akiwaahidi watanzania kuwa ujio wa muimbaji huyo umekuja kuleta faraja kubwa kwa watanzania wapenzi wa nyimbo za Injili kwani amerejea akiwa na nyimbo Bora na nzuri zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *