
Mwimbaji nyota wa muziki wa taarabu nchini Tanzania Mzee Yusuph ambaye pia ni moja ya viongozi wa Baraza la Sanaa Tanzania , ameonesha kutokubaliana na kitendo cha mwanamuziki Diamond Platnumz kukataa kushiriki katika tuzo zilizo andaliwa na serikali kupitia baraza hilo.
Mzee Yusuph amedai kuwa ni vyema kwa msanii kama Diamond Kushiriki tuzo hizo ili kutoa hamasa kwa mamia ya vijana wanaotamani kuwa wanamuziki.
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Diamond Platnumz kueleza kutotamani kushiriki katika tuzo hizo zilizo andaliwa na serikali, akidai kuwa anapenda zaidi tuzo za digital platforms za kupakua na kusikiliza muziki duniani.