
Mwigizaji kutoka Kenya Naava The Queen amepuzilia mbali madai ya kutembea kimapenzi na wanasiasa.
Hii ni baada ya walimwengu kuhoji kuwa maisha ya kifahari anayoonesha mtandaoni yanafadhiliwa na wanasiasa ambao amekuwa akitoka nao kimapenzi.
Sasa kwenye mahojiano yake mapya Naava The Queen amezima tetesi hizo kwa kusema kwamba hayana msingi wowote kwani maisha ya kifahari anayoishi ni kutokana na yeye kujituma zaidi kwenye shughuli zake za uigizaji.
Katika hatua nyingine mrembo huyo alipata umaarufu mkubwa kwenye vipindi vya runinga nchini amekanusha madai ya kufanyia mwili wake surgery ili kuboresha muonekano wake kwa kusema kuwa hajawahi jihusisha na vitendo vya kubadili muonekano wake kwa njia ya upasuaji.