
Msanii nyota nchini Nadia Mukami amefunguka sababu za kunyoa nywele zake pindi alipojifungua mtoto wake wa kwanza na Arrow Bwoy.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Nadia amesema alichukua maamuzi hayo kutokana na nywele zake kukatika kila mara alipokuwa anamnyonyosha mtoto wake.
Katika hatua nyingine ametoa wito kwa mashabiki zake wamuombee wakati huu yupo mbioni kukata uzito kutoka kilo 67 hadi 60 ili aweze kurejesha muonekano wake wa awali kabla ya kujifungua.
Kauli yake imekuja siku moja mara baada ya kukiri kuteswa na unene uliopitiliza kiasi cha kumfanya kuingiwa na uoga wa kuchapisha video pamoja na picha kwenye mitandao yake ya kijamii.