Entertainment

Nadia Mukami Atangaza Mshindi wa Woza Challenge

Nadia Mukami Atangaza Mshindi wa Woza Challenge

Msanii wa muziki nchini Kenya, Nadia Mukami, ametangaza rasmi mshindi wa Woza Challenge iliyotikisa mitandao ya kijamii kwa wiki kadhaa.

Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Nadia amesema haikuwa kazi rahisi kumchagua mshindi kutokana na ubunifu mkubwa ulioonyeshwa na washiriki wengi, lakini hatimaye Paida Mitumba aliibuka kidedea.

Kwa mujibu wa Nadia, video ya Paida Mitumba ilivutia umakini mkubwa na kufikisha watazamaji zaidi ya milioni 3 kwenye mitandao wa Tiktok, jambo lililoifanya ionekane wazi miongoni mwa video nyingi zilizoshiriki kwenye changamoto hiyo.

Nadia Mukami amewashukuru kwa dhati mashabiki walioshiriki Woza Challenge, akisema ushiriki wao umechangia pakubwa mafanikio ya wimbo huo na kuonesha nguvu ya mashabiki wa muziki Afrika Mashariki.

Wakati huohuo, video ya wimbo wa Woza inaendelea kufanya vizuri sokoni na kwa sasa inashika nafasi ya kwanza kwenye YouTube Kenya, licha ya madai kutoka kwa baadhi ya wadau wa mitandao kwamba Nadia alitumia sehemu ya wimbo wa msanii wa Tanzania Zuchu kwenye kazi hiyo. Hata hivyo, madai hayo hayajazuia Woza kuendelea kupendwa na kusikilizwa kwa wingi na mashabiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *