Entertainment

NADIA MUKAMI KUACHIA EP YAKE MPYA, ALHAMISI HII

NADIA MUKAMI KUACHIA EP YAKE MPYA, ALHAMISI HII

Msanii nyota nchini Nadia Mukami ametangaza kuachia EP mpya chini ya  lebo yake ya muziki ya Seven Hub Creatives ambayo ni zawadi kwa mashabiki zake na shukran kwa mwenyezi Mungu baada ya kujifungua salama.

EP hiyo inakwenda kwa jina la Bundle of Joy itakuwa na jumla ya nyimbo 4 ambazo amewashirikisha wakali kama Arrow boy, Latinoh na Iyanii.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Nadia Mukami ameshare artwork pamoja na Tracklist ya EP hiyo ambayo ina nyimbo kama  Zawadi, Kai wang, Acheni Mungu aitwe Mungu, na Salute kwa Mama.

Hata hivyo amewataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kupokea Bundle of Joy  EP ambayo itaingia sokoni rasmi Aprili 21 mwaka wa 2022 kupitia mtandao wa Boomplay Kenya huku akitarajia kuachia video ya wimbo wake uitwao Zawadi ambayo amemshirikisha Latinoh siku ya kesho.

Hii inaenda kuwa EP ya pili kwa mtu mzima Nadia Mukami ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2020 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo African Pop star iliyokuwa na jumla ya mikwaju 7 ya moto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *