Entertainment

Nadia Mukami mbioni kuzindua biashara yake mpya

Nadia Mukami mbioni kuzindua biashara yake mpya

Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Nadia Mukami anatarajiwa kuzindua biashara mpya katikati mwa jiji la Nairobi kando ya barabara ya Koinange mwishoni mwa wiki.

Mwimbaji huyo maarufu na mtunzi wa nyimbo ametumia ukurasa wake wa Instagram kutangaza habari hiyo njema kwa wafuasi wake wakati akizindua nembo rasmi ya saloon yake  ya urembo ambayo itakuwa inatoa huduma zake katika duka la jumla la Deluxe Mall.

Mashabiki wengi wamempongeza kwa hatua hiyo kubwa, wengine wakiulizia kama wanaweza pata kazi ambapo wengi wameahidi kuunga mkono biashara yake.

Huu umekuwa mwaka mzuri kwa Nadia, ambaye amekuwa akivunja vizingiti katika tasnia ya muziki kwa kujiboresha kwa kila njia inayoweza.

Mapema mwaka huu, alisaini msanii wake wa kwanza Latinoh, chini ya Seven Creative Hub, lebo yake ya muziki. Hii ni baada ya kutangaza kwamba anataka kupanua himaya yake kwa kusaini msanii mpya

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *